CHAD-BOKO HARAM-ONYO-USALAMA

Idriss Déby ahakikisha kujua mahali anapojificha Shekau

Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, katika video ya propaganda (picha hii ilinaswa kwenye video).
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, katika video ya propaganda (picha hii ilinaswa kwenye video). AFP

Katika mkutano na vyombo vya habari akiwa ameambatana na rais mwenziye wa Niger, Mahamadou Issoufou, Jumatano wiki hii, katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena, rais Idriss Déby ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Boko Haram na kuhakikisha kujua mahali alipokua akijificha.

Matangazo ya kibiashara

“ Tutahakikisha kuwa Boko Haram inavunjwa. Tutakabiliana na Boko Haram hadi kuhakikisha kuwa imesambaratishwa. Tuatashinda, hapana mapigano, lakini tutashinda vita dhidi ya Boko Haram, hakuna shaka”. Kauli hio ni ya rais wa Chad, Idriss Déby.

Rais wa Chad ameahidi Jumatano wiki hii katika mkutano na vyombo vya habari aliyoendesha na mwenziye wa Niger Mahamadou Issoufou, ambaye yuko ziarani Ndjamena, “ kuwasambaratisha” wanamgambo wa Boko Haram kuttoka Nigeria.

Rais wa Chad amemtaka kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, kujisalimisha mwenyewe, akibaini kwamba wanafahamu mahali alipo.

“ Akikataa kujisalimisha, atakiona cha mtimakuni”, amesema Idriss Déby.

Februari 17 mwaka huu, jeshi la Chad liliwatimua wapiganaji wa Boko Haram katika mji wa Dikwa nchini Nigeria. Wakati huo wanajeshi wawili wa Chad na wanamgambo 117 wa Boko Haram waliuawa, katika mapigano makali, jeshi la Chad limethibitisha.