LESOTHO-UCHAGUZI-SIASA

Serikali ya muungano yaundwa Lesotho

Vyama vitano vya upinzani nchini Lesotho vimeunda serikali ya muungano baada ya kushindwa kupatikana kwa mshindi wa moja kwa moja katika Uchaguzi mkuu juma lililopita.

Moja ya barabara kuu Maseru, mji mkuu wa Lesotho.
Moja ya barabara kuu Maseru, mji mkuu wa Lesotho. Photo: Michael Denne, source: Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Pakalitha Mosisili cha Democratic Congress kilipata ushindi mwembaba wa viti 47 bungeni na kuungana na vyama vingine ili kupata viti 61.

Chama cha Waziri mkuu anayeondoka madarakani Thomas Thobane All Basotho Convention kiliibuka katika nafasi ya pili kwa viti 46.

Mshindi alihitajika kupata nusu ya viti 120 vilivyokuwa vinawaniwa katika bunge la nchi hiyo ili kuunda serikali.

Uundwai wa serikali hii mpya inatarajiwa kumaliza mzozo wa kisiasa ambao umekuwa ukishuhudiwa nchini humo na hata kusababisha jaraibio la kuipundua serikali mwaka jana.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema licha ya wanasiasa kuonesha ukomavu wa hali ya juu wakati wa Uchaguzi, nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto za kisiasa.

Waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na muungano wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC wamesema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki na sauti ya wananchi wa Lesotho imesikika.