TANZANIA-MAFURIKO-USALAMA

Watu zaidi ya 40 wafariki Shinyanga

Numba nyingi za kijiji cha Mwakata ziliboka kama jengo hili la Dar es Salaam lililoanguka mwaka juzina kuua watu wawili.
Numba nyingi za kijiji cha Mwakata ziliboka kama jengo hili la Dar es Salaam lililoanguka mwaka juzina kuua watu wawili. Kwa hisani ya Ikulu ya Tanzania

Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha na wengine wasiopungua 90 kujeruhiwa katika Wilaya ya Kahama, mkoa wa Shinyanga Magharibi mwa Tanzania kutokana na mvua kubwa inayonyesha katika sehemu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mvua hiyo ya aina yakeilianza kunyesha tangu jumanne wiki hii ilisababisha nyumba 160 kuanguka na nyingine kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali na watu wengine 900 wameripotiwa kukosa makazi.

Kwa mujibu wa mkuu wa polisi katika mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, kijiji cha Mwakata kiliathirika zaidi ambako zaidi ya watu 42 walifariki na wengine 91 kujeruhiwa vibaya.

Watu wengi walifariki kutokana na kuangukiwa na kuta za udongo za nyumba za wanakijiji hao na wengine kuuawa kutokana na kuangukiwa na mawe makubwa ya barafu wakati walipokuwa wakijaribu kutafuta hifadhi baada ya mapaa kutobolewa.

Mashuhuda wamesema mawe makubwa ya barafu yalikuwa yakidondoka usiku na kuvunja nyumba za wakazi wa kijiji hicho ambazo nyingi ni za udongo.
Waokoaji walilazimika kufumua mabati yaliyoanguka na kufukua vifusi kwa ajili ya kutoa miili ya watu waliofariki na kuokoa walionusurika na baadaye kuwapakia kwenye malori na kuwasafirisha hadi hospitalini.