NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Mauaji mapya ya Boko Haram katika jimbo la Borno

Raia wa nigeria wakiukimbia mji wa Baga, katika jimbo la Borno kufuatia mashambulizi ya Boko Haram, Januari mwaka 2015.
Raia wa nigeria wakiukimbia mji wa Baga, katika jimbo la Borno kufuatia mashambulizi ya Boko Haram, Januari mwaka 2015. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI

Watu wasiopungua sitini na nane wameuawa katika kijiji cha Najba katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, katika mashambulizi yaliyotekelezwa Jumanne wiki hii na kundi la Boko Haram, maafisa wa jeshi la nchi hiyo wamethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia tukio hilo wanasema waliwaona wapiganaji hao wakiwachinja zaidi ya wanaume kumi mbele ya wake zao.

Manusura wa mashambulizi hayo walikimbilia kwenye miji jirani, miongoni mwao waliwasili katika mji wa Galma nchini Cameroon, baada ya kutembea kwa mguu mwendo wa saa sita.Vyanzo vya mashirika ya kimisaada vimebainisha.

Hata hivyo kundi la kigaidi la Boko Haram lilitekeleza hivi karibuni mashambulizi katika mji wa Gwoza Kaskazini mwa nchi hiyo na kusababisha vifo zaidi ya watu 60 wengi wao wakiwa watoto.

Licha ya mauaji haya, je jeshi la muugano kutoka Nigeria, Cameroon, Chad na Niger unafanikiwa dhidi ya Boko Haram, na uchaguzi unaweza kuathirika katika eneo hilo mwisho wa mwezi huu.