Rais Kafando atolea wito jeshi kuwa na mshikamano
Imechapishwa:
Rais mpito wa Burkina Faso, Michel Kafando amekutana Alhamisi katika Ikulu na vikosi vya jeshi, ambapo amevitolea wiko kuwa na umoja na nidhamu.
Rais Kafando amelitaka jeshi kuwa na umoja na mshikamano bila kuwa na upendeleo au kuegemea upande wowote, na kujitenga mbali na masuala ya siasa.
Hayo yakijiri, serikali ya Burkina Faso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara . Jambo ambalo serikali hiyo ilisema italiangazia suala hilo wakati ilipochukua madaraka.
Watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Jijini Paris Nchini Ufaransa, Mjane wa marehemu Bi Miriam, amesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la Mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji ya mume wake.
Bwana Sankara aliuawa mwaka 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaoré kuchukua mamlaka.
Blaise Campaoré aliondolewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.