NIGERIA-MASHAMBULIZI-USALAMA

Maiduguri yakumbwa na mashambulizi matatu

Vikosi vya usalama vikitafuta dalili katika mlango wa soko ya Monday market katika mji wa Maiduguri, ambapo kulitokea moja ya milipuko iliyoutukisa mji huo, Machi 7 mwaka 2015.
Vikosi vya usalama vikitafuta dalili katika mlango wa soko ya Monday market katika mji wa Maiduguri, ambapo kulitokea moja ya milipuko iliyoutukisa mji huo, Machi 7 mwaka 2015. AFP / PTUNJI OMIRIN

Mji wa Maiduguri, ambako lilianzishwa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria, umeshambuliwa Jumamosi Machi 7 kwa mashambulizi matatu yanayodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kiislamu, shambulio ambalo liligharibu maisha ya takribani watu 58 na 139 wamejeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi mawili yametekelezwa na watu waliojitoa mhanga. Watoto kadhaa wameuawa katika mashambulizi hayo, ambayo yanadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram. Masoko mawili yanatotembelewa na watu wengi pamoja na kituo cha magari, ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambulia.

Shambulio la kwanza limetokea saa nne na dakika 20 saa za kimataifa, wakati mtu alijitoa mhanga na kujilipua akitumia vilipuzi alivyokua amevalia katika soko la samaki katika mji wa Baga. Shambulio hilo liligharimu maisha ya watu 18, kwa mujibu wa Abubakar Gamandai, mmoja wa viongozi wa chama cha wavuvi katika jimbo la Borno lenye mji mkuu Maiduguri.

Saa moja baadae, mlipuko mwingine ulipiga soko la pili la Maiduguri, Monday Market, na kugharimu maisha ya watu 15 na kusababisha hali ya sintofahamu. Shambulio la tatu liendeshwa dhidi ya kituo cha magari kinachotembelewa na watu wengi. Baadhi ya mashahidi wamebaini kwamba mashambulizi haya mawili ya mwisho yalitekelezwa na watu waliojitoa mhanga, lakini taarifa hii haikuweza kuthibitishwa.

Jeshi la Nigeria lalaumiwa

Kulingana na idadi iliyotolewa na mkuu wa polisi katika jimbo la Borno, Clement Adoda, takribani watu 58 wameuawa katika mashambulizi hayo na wengine 139 wamejeruhiwa. Viongozi wameamuru kufungwa kwa shughuli zote za biashashara katika mji wa Maiduguri kutokana na mashambulizi hayo, ambapo wengi wamehofia kutokea kwa mashambulizi mengine.

Jeshi la Nigeria ambalo limelaumiwa kutoonyesha bidii ya kuwatimua wanamgambo wa Boko Haram, limetangaza kwamba limeiweka chini ya udhibiti wake baadhi ya miji katika majuma ya hivi karibuni kwa usaidizi wa majeshi kutoka nchi jirani (hususan Chad, lakini pia Cameroon na Niger) pamoja na majeshi kutoka nchi za Magharibi ( Ufaransa, Canada, Marekani,...) ambayo yanapiga kambi kwenye mpaka kaskazini mwa Nigeria.