MALI-UFARANSA-UGAIDI-USALAMA

Shambulio dhidi ya mgahawa mmoja Bamako

AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Mgahawa mmoja katika moja ya kata za Bamako inayotembelewa mara kwa mara na watu kutoa nchi za Magharibi ulishambuliwa kwa risasi usiku wa Ijumaa Machi 6 kuamkia Jumamosi 7.

Matangazo ya kibiashara

Watu watano wameuawa, ikiwa ni pamoja na raia watatu wa Mali, raia mmoja wa Ufaransa na raia mwengine mmoja kutoka Ubelgiji.

Watu tisa wamejeruhiwa katika shambulio hilo, ikiwa ni pamoja na wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na kupiga vita dhidi ya mabomu yanayotegwa ardhini, kwa mujibu wa taarifa kutoka Minusma.

Ni kwa mara ya kwanza tukio kama hili ambalo lilisababisha maafa kutokea katika mji mkuu wa Mali, Bamako, tangu kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa kutumwa nchini humo.

Shambulio hilo limetokea siku moja baada ya shambulio jingine kutokea katika mji wa Bamako katika mtaa unaitwa “ Princesse”, ambao unatembelea na raia wa nchi za Magharibi.

Wakati huohuo marais wa Ufaransa na Mali wameamua kuchukua hatua za pamoja kwa kuimarisha usalama nchini Mali, kwa mujibu wa Ikulu ya Elysée.

Baada ya shambulio hilo lililogharimu maisha ya watu watano, rais wa Ufaransa François Hollande, amezungumza na mwenziye Ibrahim Boubacar Keïta. " Rais Hollande amemueleza mwenziye wa Mali kwamba Ufaransa inaunga mkono katika kupambana dhidi ya ugaidi nchini Mali”, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Elysée. Marais hao wawili wametathmini utaratibu wa ushirikiano kuhusu uchunguzi ambao umeanza.