NIGER-CHAD-NIGERIA-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI-USALAMA

Mashambulizi makubwa yaanzishwa na Niger pamoja na Chad

Mji wa Diffa kwenye mpaka na Niger, unapatikana kwenye umbali wa kilomita 7 na Nigeria. Mashambulizi yanaendeshwa katika jimbo la Borno, Nigeria na wanajeshi wa Chad pamoja na Niger walivuka mpaka karibu na mji wa Diffa.
Mji wa Diffa kwenye mpaka na Niger, unapatikana kwenye umbali wa kilomita 7 na Nigeria. Mashambulizi yanaendeshwa katika jimbo la Borno, Nigeria na wanajeshi wa Chad pamoja na Niger walivuka mpaka karibu na mji wa Diffa. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI

Majeshi ya Niger pamoja na Chad yameanzisha Jumapili Machi 8 mashambulizi makubwa ya angani na ardhini nchini Nigeria dhidi ya Boko Haram, siku moja baada ya kundi la Boko Haram kutangaza “kutii” kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yameanzia kusini mashariki mwa Niger.

Majeshi ya Chad na Niger yanayopiga kambi kusini mashariki mwa Niger yameendesha mashambulizi mapema Jumapili Machi 8 dhidi ya ngome za kundi la Boko Haram katika ardhi ya Nigeria. Mashambulizi haya ambayo yameanzishwa ni ufunguzi wa mapigano ya tatu katika ardhi ya Nigeria.

Vikosi vya Chad na Niger vimevuka daraja la Doutchi ambalo linaunganisha Niger na nigeria kwenye saa mbili asubuhi, Dakika chache baadae, makombora na zana nzitonzito za kijeshi vimesikika na baadae vimeendelea kusikika kwa mbali kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele, mashahidi wameeleza.

Chanzo cha kijeshi kimebaini kwamba kabla ya shambulio la ardhini, ndege za kijeshi zilianza “ kukagua adui” kwa muda wa saa 48. Mapigano bado yanaendelea, na ni mapema mno kueleza hasara iliyotokea katika mashambulizi hayo, uongozi wa jeshi la Chad umebaini.

Mashambulizi haya yalioandaliwa na majeshi kutoka nchi za Chad na Niger tangu majuma kadhaa yaliyopita, yanapelekea majeshi ambayo yamepiga kambi kwenye mpaka kukabiliana na adui. Magari na vifaru zaidi ya 200 vinatumiwa katika mashambulizi haya yanayoendelea dhidi ya Boko Haram.