TANZANIA-ALBINO-HAKI-SHERIA-USALAMA

Malbino waandelea kushambuliwa Tanzania

Matukio ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini Tanzania baada ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono.

Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wanakabiliwa na mauaji na visa vya utekaji nyara. Waganga wa kienyeji wanyooshewa kidole kwa kutumia viongo vya watu hao  katika imani za kishirikina, à Dar-es-Salaam, Mei 5 mwaka 2014.
Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wanakabiliwa na mauaji na visa vya utekaji nyara. Waganga wa kienyeji wanyooshewa kidole kwa kutumia viongo vya watu hao katika imani za kishirikina, à Dar-es-Salaam, Mei 5 mwaka 2014. PHOTO/MILLIYET DAILY HANDOUT/BUNYAMIN AYGUN
Matangazo ya kibiashara

Visa vya mauaji na ukatili vimeendelea kuwalenga watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania. Mtoto wa miaka tisa mwenye ulemavu wa ngozi, ameponea kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kukatwa kiganja cha mkono nyumbani kwao.

Mtoto huyo huyo ambaye ni mvulana alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.

Shambulio hilo jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa Tanzania.

Tukio hilo ni la tatu kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja baada ya kuibuka kwa matukio mengine mawili ya watoto walemavu wa ngozi katika mkoa wa Mwanza na Geita. Pendo Emmanuel mkazi wa Ndami wilayani Kwimba mkoani Mwanza pamoja na Yohana Bahati, mkazi wa Ilelema wilayani Chato mkoani Geita, ambao ni walemavu wa ngozi walitekwa hivi karibuni kwa nyakati tofauti.

Yohana alitekwa Februari 15 mwaka 2015, aliokotwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umekatwa mikono na miguu na kisha kufukiwa kwenye shimo.

Kamanda wa polisi katika mkoa wa Rukwa, Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.

Polisi imeanzisha uchunguzi ili kuwafichua waliohusika na kitendo hiki cha kikatili.

Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alivchukua uamzi wa kuwafutia vibali waganga wa kienyeji huku wenzao 32 wakishikiliwa na polisi kutokana na kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Hata hivyo chama cha waganga wa Tiba Asilia Tanzania (Chawatiata) tawi la mji wa Katoro wilayani Geita, kimeomba Serikali kuwachukulia hatua kali wanaobainika kuhusika na vitendo hivyo badala ya kuwafutia vibali waganga wote.

Viongozi wametishia kuwafutia vibali waganga wa kienyeji, baada ya kubainika kwamba waganga hao wamekua wakitumia viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina.
Hivi karibuni wanachama wa chama hicho walikutana juzi kuzungumzia tuhuma dhidi yao ya kuhusishwa na mauaji ya albino. Walisema wasihukumiwe kwa ujumla badala yake uchunguzi wa kina ufanywe kubaini wahusika.