COTE D'IVOIRE-SIMONE-SHERIA

Simone Gbagbo ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Simone Gbagbo,mke warais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo (kushoto) amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela
Simone Gbagbo,mke warais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo (kushoto) amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela AFP PHOTO / SIA KAMBOU

Mke wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Simone Gbagbo, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi kati ya mwaka 2010 na 2011 nchini Côte d’Ivoire.

Matangazo ya kibiashara

Watu 3000 waliuawa katika machafuko hayo. Michel Gbagbo, mtoto wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela na kunyimwa haki zake za kiraia.

Kifungo hicho cha miaka 20 jela alichopewa Simone Gbagbo ni adhabu kubwa ikilinganisha na ile aliyoiomba mwanasheria wa serikali wakati kesi hiyo ilipokua ikisikilizwa. Wakati huo mwanashria wa serikali alimuombea Simone Gbagbo kifungo cha miaka 10 jela. Adhabu hiyo imejulimshwa mara mbili.

Maafisa wawili wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na Vagba Faussignaux na jenerali Brunot Dogbo Blé, mkuu wa kikosi kilichokua kikitoa ulinzi wa taasi za nchi wamehumiwa pia kifungo cha miaka 20 jela na kunyimwa haki zao za kiraia.

Uamzi huo ulisubiriwa kuanzia saa tisa alaasiri hadi saa sita usiku Jumatatu wiki hii.

Kwa upande wake mwanasheria wa Simone Gbagbo amelani hukumu hiyo dhidi ya mteja wake, akibaini kwamba majaji hawakua huru katika kesi hiyo, huku akisema kuwa majaji wameshawishiwa na baadhi ya viongozi srikalini.

Mwanasheria wa serikali, Soungalo Coulbaly, amesema ameridhishwa na hukumu hiyo dhidi ya Simone Gbagbo.

“ Nadhani kwamba hukumu hiyo inaeleweka, kwani Simone Gbagbo alihusika katika machafuko yaliyogharimu maisha ya watu wengi nchini Côte d’Ivoire. Uamzi huu unaturidhishwa kwa kweli, kwani waathirika watafurahi kuona wametendewa haki”, amesema Coulbaly.

Hata hivyo mawakili wa watuhumiwa wamesema watakata rufaa.