COTE D'IVOIRE-SIMONE-SHERIA

HRW yalaani uamzi wa Mahakama dhidi ya Simone Gbagbo

Simone Gbagbo à son arrivée à la cour d'assises d'Abidjan, lundi 23 février 2015.
Simone Gbagbo à son arrivée à la cour d'assises d'Abidjan, lundi 23 février 2015. AFP/ISSOUF SANOGO

Baada ya Mahakama ya Côte d’Ivoire kutoa umazi wake dhidi ya mke wa zamani wa rais wa Côte d’Ivoire, Simone Gbagbo, Shirika la kuimataifa la haki za binadamu Human Right Watch limebaini kwamba keshi hiyo iliyokua ikiendeshwa dhidi ya watuhumiwa 80 "haikuendeshwa kulingana na viwango vya sasa katika kesi zinazofuata sheria".

Matangazo ya kibiashara

Lakini, kwa mujibu wa Jean-Marie Mzigo, mkurugenzi wa Ofisi ya Human Right Watch nchini Ufaransa, " hukumu ya Simone Gbagbo haimaanishi kwamba haki imetendeka kwa waathirika wa machafuko yaliyoikumba Côte d’Ivoire kati ya mwaka 2010 na 2011”.

 

Mwezi Desemba mwaka 2014, Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ilibaini kwamba Côte d’Ivoire haingiweza kutoa hukumu ya haki kwa Simone Gbagbo na kuomba kwa mara nyingine atumwe mjini Hague. Wakati huo Serikali ya Côte d’Ivoire ilikata rufaa. Uamzi mpya unasubiriwa.

Kwa upande wa kambi ya Laurent Gbagbo umebaini kwamba kesi hiyo iligubikwa na dhulma.

Simone Gbagbo, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi kati ya mwaka 2010 na 2011 nchini Côte d’Ivoire.

Watu 3000 waliuawa katika machafuko hayo. Michel Gbagbo, mtoto wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela na kunyimwa haki zake za kiraia.

Kifungo hicho cha miaka 20 jela alichopewa Simone Gbagbo ni adhabu kubwa ikilinganisha na ile aliyoiomba mwanasheria wa serikali wakati kesi hiyo ilipokua ikisikilizwa. Wakati huo mwanashria wa serikali alimuombea Simone Gbagbo kifungo cha miaka 10 jela. Adhabu hiyo imejulimshwa mara mbili.

Maafisa wawili wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na Vagba Faussignaux na jenerali Brunot Dogbo Blé, mkuu wa kikosi kilichokua kikitoa ulinzi wa taasi za nchi wamehumiwa pia kifungo cha miaka 20 jela na kunyimwa haki zao za kiraia.

Hata hivyo mawakili wa watuhumiwa wamesema watakata rufaa.