Joyce Aluoch makamu mwenyekiti wa ICC
Imechapishwa: Imehaririwa:
Jaji Joyce Aluoch, ambaye ni raia wa Kenya amechaguliwa kama makamu mwenyekiti wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.
Joyce Aluoch atahudumu kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu. Joyce Aluoch anashikilia wadhifa huo kufuatia uchaguzi uliyopigwa Jumatano wiki hii na majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita.
Judge Fernández de Gurmendi elected #ICC President; Judges Aluoch & Ozaki as Vice-Presidents http://t.co/KzEO7NJifq pic.twitter.com/PQ5S2C15RX
— Int'l Criminal Court (@IntlCrimCourt) March 11, 2015
Jaji Silvia Fernandez de Gurmendi kutoka Argentina amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa ICC, naye jaji Kuniko Ozaki kutoka Japani, amechaguliwa kuwa makamu wa pili wa mwenyekiti wa ICC.
Mwenyekiti pamoja na wamakamu wake wawili wanaunda kile kinachojulikana kama bodi ya uwenyekiti wa Mahakama ya ICC, na bodi hiyo ndio hutoa mwongozo wa Mahakama kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Mahakama ni mratibu wa Mahakama na vitengo vingine vilivyo chini ya mamlaka ya ICC.
Mwenyekiti wa Mahakama ya ICC ana madaraka kamili, bila kuingiliwa kwa kazi yake wala kushirikiana katika kazi yake na kiongozi wa Mashtaka.