CAR-SELEKA-USALAMA-SIASA

Kiongozi wa kundi la waasi wa zamani la Seleka akamatwa

Waasi wa zamani wa Seleka wameghadhabishwa na kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo la zamani la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wanajeshi wa kundi la zamani la waasi la Seleka wakiwa katika gariaina ya Pickup, kaskazini mwa mji wa Bangui, Januari 27 mwaka 2014.
Wanajeshi wa kundi la zamani la waasi la Seleka wakiwa katika gariaina ya Pickup, kaskazini mwa mji wa Bangui, Januari 27 mwaka 2014. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Ousmane Mahamat Ousmane, ambaye ni naibu kiongozi wa vuguvugu la waasi wa zamani wa Seleka ambao walibadili jina na kuitwa FPRC, alikamatwa mwishoni mwa juma lililopita, baada ya kuiingia na kikosi cha walinzi wake katika uwanja wa ndege wa Bangui.

FPRC imeomba kiongozi huyo aachiliwe huru mara moja ili aweze kushiriki katika mkutano wamaridhiano mjini Bangui.

Kiongozi huyo wa kundi la zamani la waasi la Seleka, alikamwata wakati alikua alikuja kumtafuta mke wake katika uwanja wa ndege wa Bangui, na kikosi chake cha ulinzi kilipokonywa silaha.

“ Bwana Ousmane Mahamat Ousmane, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Bangui Mpoko, wakati ambapo alikua akishindikizwa na kundi la watu wenye silaha, ambao waliokua wakivalia sare ya jeshi”, mwendesha mashtaka katika Mahakama ya jiji la Bangui, Gislain Grezenguet, amethibitisha.

Viongozi wa kisiasa wa FPRC wamechukulia kitendo hiki cha kukamatwa kwa kiongozi wao kama uchokozi. Wamebaini kwamba Ousmane Mahamat Ousmane, alikua na haki ya kushindikizwa na watu wenye silaha kwa ajili ya usalama wake.