NIGERia-CHAD-NIGER-BOKO HARAM-Usalama

Damasak Bado mikononi mwa Boko Haram

Jeshi la Cha lapiga doria Nigeria dhidi ya Boko Haram, Februari 3 mwaka 2015.
Jeshi la Cha lapiga doria Nigeria dhidi ya Boko Haram, Februari 3 mwaka 2015. AFP / STEPHANE YAS

Wanajeshi wa Chad na Niger bado hawajaudhibiti mji wa Damasak, ambao unaendela kushikiliwa na kundi la Boko haram.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo kutoka Chad vilithibitisha hivi karibuni kwamba majeshi ya Chada na Niger yanaudhibiti mji wa Damasak, katika jimbo la Borno, nchini Nigeria, kwenye umbali wa kilomita kadhaa kusini mwa mpaka na Niger, Taarifa hiyo imekanushwa Jumatano wiki hii na wanajeshi kadhaa wa Niger.

Vyanzo vya kijeshi vya Niger vimebaini kwamba mapigano makali yamekua yakishuhudiwa tangu Jumapili Machi 9 kati ya jeshi la Niger na wanamgambo wa Boko Haram.

Mapigano makali yalishuhudiwa Jumapili. Wanajeshi kadhaa wa Nigeria walijeruhiwa na zaidi ya kumi waliuawa upande wa jeshi la Chad, kwa mujibu wa chanzo cha usalama cha Chad ambacho kimenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Majeshi kutoka nchi hizi mbili ambayo yanaongozwa na jenerali kutoka Chad bado hayajaingia katika mji wa Damasak, lakini yamekua yakiendelea na mapigano dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram katika baadhi ya vijiji viliyo pembezoni mwa mji wa Damasak.