SOMALIA-AL SHABAB-MAPIGANO-Usalama

Serikali ya mkoa wa Baïdoa yashambuliwa na Al Shabab

Msemaji wa Al Shabab kutoka Somalia, Sheikh Ali Mohamud Rage, Februari 13 mwaka 2012.
Msemaji wa Al Shabab kutoka Somalia, Sheikh Ali Mohamud Rage, Februari 13 mwaka 2012. AFP PHOTO / Mohamed Abdiwahab

Mji wa Baïdoa, kusini mwa Somalia, ulishuhudia shambulio linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Al Shabab mapema Alhamisi asubuhi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vikosi vya usalama, watu wenye silaha wameendesha shambulio dhidi ya makao makuu ya serikali ya mkoa wa Baïdoa, uwanja wa ndege, makao makuu ya kikosi cha Umoja wa Afrika na ofisi za Umoja wa Mataifa.

Vyanzo vya usalama viliyonukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, vimebaini kwamba watu watano waliokua wakivalia sare ya jeshi waliwapiga watu kabla ya kuingia katika jengo kunako fanyia kazi serikali.

Takribani watu watano wameuawa katika shambulio hilo. Kulingana na waziri wa usalama katika eneo hilo washambuliaji 3 waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi ya kikosi cha jeshi la Somalia waliuawa baada ya majibizano ya risasi ambayo yaliendelea kwa takribani dakika 20.

Maafisa wawili wa usalama waliuawa huku raia wawili pia wakijeruhiwa.

Vyanzo vya usalama vimearifu kuwa mashambulizi hayo yalianza kwa mlipuko katika lango la makao hayo kabla milio ya risasi kusikika ndani ya jengo hilo.