BURUNDI-UNSC-SIASA-USALAMA

UNSC yamuonya Nkurunziza kutogombea katika uchaguzi ujao

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao umekua ziarani mjini Bujumbura, nchini Burundi umemuonya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutogombea katika uchaguzi wa urais ujao.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ambaye bBaraza la Usalam ala Umoja wa Mataifa limemtaka kutogombea katika uchaguzi wa urais.ujao
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ambaye bBaraza la Usalam ala Umoja wa Mataifa limemtaka kutogombea katika uchaguzi wa urais.ujao AFP PHOTO/Brendan SMIALOWSKI
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo umesema umemuonya rais Nkurunziza ili kuzuia machafuko ambayo yanaweza kutokea kutokana na kugombea kwake kwa muhula watatu.

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umebaini kwamba rais Pierre Nkurunziza ameshagombea mara mbili, na hivyo hawezi kugombea muhula watatu.

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umesema Mkataba wa Arusha na katiba ya nchi vinapaswa kuheshimishwa kwa faida ya taifa la Burundi na wananchi wake kwa ujumla.

Katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa jioni wiki hii, ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umesema kuwa umemsihi rais Nkurunziza kutokwenda kinyume na Mktaba wa Arusha na Katiba ya nchi, ambavyo vinaweka wazi muda ambao rais anatakiwa kuwa madarakani.

Awali kabla ya mkutano kati ya ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari, waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana, amefahamisha kwamba ziara ya ujumbe huo nchini Burundi haiambatani na suala ya mihula ya rais Nkurunziza, akibani kwamba katika agenda ya mazungumzo na rais, suala hilo halitajadiliwa.

Ujumbe huo umesema kushangazwa na kauli ya waziri Edouard Nduwimana.

Ujumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umekutana na wadau wote katika mchakato wa uchaguzi nchini Burundi.

Hivi karibuni Mareakni, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika pamoja na shirika la marais wastaafu barani Afrika, linaloongozwa na Koffi Anan, vilimtaka rais Pierre Nkurunziza kutogombea katika uchaguzi wa urais ujao.