MAREKANI-SOMALIA-KENYA -USALAMA

Marekani yatathmini kuhusu shambulizi la anga nchini Somalia

Wanamgambo wa Alshabab nchini Somalia wanapambana kuondoa utawala wa Somalia na kuweka serikali ya kiislamu
Wanamgambo wa Alshabab nchini Somalia wanapambana kuondoa utawala wa Somalia na kuweka serikali ya kiislamu

Jeshi la Marekani linaathimini matokeo ya shambulizi la anga dhidi ya kiongozi mkubwa wa kundi la Alshabab nchini Somalia, Penthagon imearifu.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Marekani linaathimini matokeo ya shambulizi la anga dhidi ya kiongozi mkubwa wa kundi la Alshabab nchini Somalia Penthagon imearifu.

Oparesheni hiyo ambayo haikuhusisha jeshi la Marekani kwa upande wa ardhini ilifanyika alhamisi katika barabara ya kusini mwa Mogadishu kumlenga kiongozi muhimu wa alshabab kwa mujibu wa maelezo ya msemaji kanali Steven Warren.

Oparesheni hii ililenga kusambaratisha mtandao wa kigaidi wa alshabab.

Hata hivyo kundi la Wanamgambo wa Somalia wa Al-Shabab limetekeleza shambulio la kushtukiza dhidi ya msafara wa maofisa wa Serikali ya Kenya kwenye mpaka wa nchi hiyo na Kenya ambapo watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa.

Kwenye msafara huo alikuwepo pia gavana wa Kaunti ya Mandera, Ali Roba ambaye alinusurika kwenye shambulio hili ambalo watu sita walijeruhiwa vibaya, hii ni kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya.

Tayari kundi la Al-Shabab limekiri kuhusika kwenye shambulio hili, ambalo limezusha upya hofu ya wananchi kuhusu usalama wao katika mji wa Mandera.