Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Wakati joto la uchaguzi likizidi kupanda Hussein Rajabu ajitokeza, DRC pia Umoja wa mataifa walaumu maafisa 7 wa jeshi kuhusika na ukiukaji wa Haki za binadamu

Sauti 21:43

Katika makala hii wiki hii tunaangazia Uchaguzi wa Rais na Wabunge nchini Burundi unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei na Juni mwaka huu. Kutokana na kuendelea kwa mchakato wa uchaguzi joto la kisiasa limeendelea kupanda huku aliyekuwa Kiongozi wa chama tawala cha CNDD FDD Hussein Rajabu, akajitokeza juma hili na kuzungumzia namna ambavyo aliondoka jela, na kuwaonya warundi kuwa makini kuhusu Uchaguzi.Pia katika makala haya tumeangazia hatua ya serikali ya Uganda kupiga marufuku ukahaba, wakati huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, umoja wa mataifa kuwalaumu wanajeshi saba kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.Ungana nami Reuben Lukumbuka katika makala haya.