NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Boko Haram yateketeza kwa moto nyumba kadhaa Bama

Askari polisi wa Nigeria katika mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno, Nigeria, katika operesheni dhidi ya Boko Haram, mwezi Juni 2013.
Askari polisi wa Nigeria katika mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno, Nigeria, katika operesheni dhidi ya Boko Haram, mwezi Juni 2013. AFP PHOTO / Quentin Leboucher

Nchini Nigeria, kundi la kigaidi la Boko Haram limeteketeza makaazi ya watu katika mji wa Bama Kusini Mashariki mwa mji wa Maiduguri. 

Matangazo ya kibiashara

Mji wa Bama umekuwa ukidhibitiwa kwa muda mrefu na kundi hilo, na kabla ya makaazi hayo kuteketezwa moto, wenyeji walialazimishwa kuondoka.

Hatua hiyo ya Boko Haram imesabisha mamia ya watu kukimbilia mjini Maiduguri kwa kuhofia usalama wao.

Umar, mmoja wa waakazi wa mji wa Bama ameliambia Shirika la Habari la Ufransa AFP kuwa wanamgambo hao waliwaonya wakaazi hao kuwa ikiwa wangekataa kuondoka wangeuawa.

Wanawake na watoto wameonekana wakitembea kwa miguu,
wakiacha makaazi yao yakichomwa moto bila ya kuambiwa ni kwanini hatua hiyo inachuliwa na magaidi hao.

Mji huo wa Kihistoria katika jimbo la Maiduguri umekuwa ukidhibitiwa na Boko Haram tangu mwezi Septemba mwaka jana.

Jeshi la pamoja kutoka Chad, Cameroon na Niger limeendeleza mashambulizi dhidi ya kundi hilo katika maeneo mengine Kaskazini mwa nchi hiyo ambayo inaelekea katika uchaguzi mkuu tarehe 28 mwezi huu.