NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Jeshi la Nigeria lajigamba dhidi ya Boko Haram

Wanajeshi wa Nigeria katika mji wa Baga. Jeshi la Nigeria lathibitisha kwamba limeutwaa mji wa Bama.
Wanajeshi wa Nigeria katika mji wa Baga. Jeshi la Nigeria lathibitisha kwamba limeutwaa mji wa Bama. REUTERS/Tim Cocks

Jeshi la Nigeria limesema limewatokomeza wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Yobe.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Nigeria limesema pia kuwa limeukomboa mji wa Bama katika jimbo la Borno uliokua ukidhibitiwa kwa kipindi kirefu na na Boko Haram.

Msemaji wa jeshi la Nigeria Chris Olukolade katika ukurasa wake wa Twitter amesema, jeshi la Nigeria limefanikiwa kuukomboa mji wa mwisho uliokuwa unakaliwa na magaidi hao.

Haya ni mafanikio makubwa kwa jeshi la Nigeria ambalo limekuwa likipata msaada kutoka kwa majeshi ya Chad, Cameroon na Niger kuwaongamiza wanamgambo wa Boko Haram katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe.

Nigeria inajiandaa kwa Uchaguzi mkuu tarehe 28 mwezi huu na serikali iliahidi kuwa kabla ya uchaguzi huo kundi hili la Boko Haram litakuwa limetokomezwa.