TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Beji Caid Essebsi aapa kutokomeza ugaidi

Maafisa wa jeshi la Tunisia walioijificha nyuso zao wakiwa karibu ya kukabiliana na magaidi waliovamia makavazi ya Bardo jijini Tunis, Machi 18 mwaka 2015.
Maafisa wa jeshi la Tunisia walioijificha nyuso zao wakiwa karibu ya kukabiliana na magaidi waliovamia makavazi ya Bardo jijini Tunis, Machi 18 mwaka 2015. REUTERS/Zoubeir Souissi

Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi anasema nchi yake ipo kwenye vita na ugaidi, na itapambana bila huruma kuwaangamiza magaidi katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya rais Essebsi inakuja baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kuwateka nyara watalii katika makavazi ya Bardo jijini Tunis Jumatano wiki hii.

Watu 21 wakiwemo wauwaji 2 waliuawa katika makabiliano kati ya magaidi hao na polisi waliokuwa wanajaribu kuwaokoa watalii hao, kutoka Japan, Italia, Colombia, Australia, Ufaransa, Poland na Uhispani. Watu wengine zaidi ya 40 walijeruhiwa katika makabiliano hayo.

Vyanzo vya kiusama vimebaini kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka, kwani kuna majruhi ambao wako katika hali mbaya.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameahidi kushirikiana na Tunisia kupamabana dhidi ya ugaidi.

Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje, John Kerry amelaani shambulio hilo la kigaidi , akibaini kwamba ugaidi hauna nafasi katika ulimwengu huu.

Kundi moja la kigaidi lilijigamba kuendesha shambulio hilo na kupongeza wanamgambo wake waliloliendesha.