NIGERIA-NIGER-CHAD-BOKO HARAM-USALAMA

Damasak mikononi mwa majeshi ya Chad na Niger

Bendera iliyopokonywa kutoka mikononi mwa vikosi vya Boko Haram, ikishikiliwa na anajeshi wa Niger, ambao wameingia katika mji wa Damasak, nchini Nigeria, Machi 18 mwaka 2015. Majeshi ya  Chad na Nigeria yanashiriki katika mashambulizi dhidi ya askari ya v
Bendera iliyopokonywa kutoka mikononi mwa vikosi vya Boko Haram, ikishikiliwa na anajeshi wa Niger, ambao wameingia katika mji wa Damasak, nchini Nigeria, Machi 18 mwaka 2015. Majeshi ya Chad na Nigeria yanashiriki katika mashambulizi dhidi ya askari ya v REUTERS/Emmanuel Braun

Majeshi ya Chad na Niger yametangaza mwanzoni mwa wiki hii kwamba yaliudhibiti mji wa Damasak, nchini Nigeria.  

Matangazo ya kibiashara

Majeshi hayo yalitangaza Machi 8 mwaka 2015 kwamba yaliuteka mji wa Damasak kabla ya kukanusha taarifa hiyo. Kulingana na idadi iliotolewa na jeshi la Niger, mapigano kati ya majeshi hayo na Boko Haram yamegharimu maisha ya watu 300.

Vilipokua vikivuka mto Komadougou Yobé Machi 8, vikosi vya Chad na Niger havikutaraji upinzani kutoka Boko Haram. Kanali Ahmat Youssouf wa jeshi la Chad amesema ameelezea jinzi walivyopigana kwa minajili ya kuudhibiti mji wa Damasak.

“ Tulipigana kwa vita ya kwanza baadae vita ya pili, karibu na maeneo yalio karibu kabla ya kufika Damasak”, amesema afisa huyo.

Kanali wa jeshi la Niger ameieleze RFI matatizo yalisababishwa na hali mbaya ya mazingira.

Majeshio hayo kutoka Chad na Senegal yametangaza kuwa yamewatolea wito raia ambao waliyakimbia makaazi yao kurudi makwao. Hata hivyo majeshi hayo ya muungano yameapa kuendelea na mapambano hadi sehemu ambako adui amekimbilia.