SIERRA LEONE-SIASA

Sierra Leone : Sam-Sumana afutwa kazi

Rais wa Sierra Leone  Ernest Bai Koroma na Makamu wake Samuel Sam-Sumana, Freetown mwezi Oktoba mwaka 2012.
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma na Makamu wake Samuel Sam-Sumana, Freetown mwezi Oktoba mwaka 2012. REUTERS/Simon Akam/Files

Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma amemfuta kazi Makamu wake wa rais Samuel Sam-Sumana kwa kuomba hifadhi ya kisiasa katika ubalozi wa Marekani jijini Freetown juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka katika Ikulu ya Freetown zinasema rais Koroma amesema amechukua uamizi huo baada ya Sumana kuacha majukumu yake na kuomba hifadhi katika ubalozi wa nchi ya kigeni.

Koroma amesema kuwa atamteua Makamu mwingine wa rais kuchukua nafasi ya Sumana ambaye pia amefukuzwa katika chama tawala cha APC.

Hata hivyo, wakili wa Sumana, Blyden Jenkins-Johnson, amesema wanajadiliana kuhusu uamuzi huo wa rais Koroma kabla ya kuchukua uamuzi.

Uongozi wa chama tawala ulimwondoa katika chama hicho baada ya kudai kuwa alikuwa ameunda mrengo mwingine ndani ya chama, tuhma ambazo Sumana alikanusha.

Mapema juma hili, Koroma alijitikeza na kukanusha taarifa kuwa alikuwa ameoomba hifadhi ya kisiasa katika ubalozi wa Marekani.