DRC-BURKINA FASO-SENEGAL-SHERIA-DIPLOMASIA

Wanaharakati kutoka Senegal na Burkina Faso wafukuzwa DRC

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende.
Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH

Wanaharakati kutoka nchini Senegal na Burkina Faso waliotiwa mbaroni mwishoni mwa juma lililopita mjini Kinshasa wamefukuzwa na kurejeshwa makwao.

Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao waliondoka jijini Kinsasha Jumatano usiku wiki hii wakiwa ndani ya ndege ya shirika la Brussels Airlines walibadilishiwa ndege na kuondoka na ndege ya shirika la Uturuki.

Awali Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende, alioiambia RFI kwamba wanaharakati hao watafukuzwa nchini humo kulingana na amri ya Rais Joseph Kabila.

Hatua ya kuwafukuza wanaharakati hao inaenda sanjari na ombi la rais wa Senegal Macky Sall, ambaye alimuomba mwenzake wa Congo Joseph Kabila kuwaachia huru wanaharakati hao, huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka jumuiya ya kimataifa kutaka watu hao waachiwe huru.

Hata hivyo, wanaharakati 17 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliokamatwa pamoja na wenzano wa Senegal na Burkina Fasso bado wanazuiliwa wakisubiria kufunguliwa mashtaka kama alivyotangaza Jumatano wiki hii waziri Mende.