LIBERIA-SIERRA LEONE-GUINEA, EBOLA-AFYA

Ebola: raia watakiwa kubaki makini Afrika Magharibi

Wakati ambao liberia imeorodhesha mtu mmoja kubainika na virusi vya Ebola, Jumamosi mwishoni mwa juma hili, rais wa Sierra Leone, nchi ambayo ni jirani ya Liberia, amewataka raia wake kukutana kwa mazungumzo kwa muda wa siku tatu kuanzia Machi 27.

RFI/Sébastien Nemeth
RFI/Sébastien Nemeth RFI/Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Licha ya nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola kukabiliwa na hali mbaya, viongozi wa mataifa hayo wamewataka raia wao kuwa makini.

Kwa mujibu wa viongozi wa Sierra Leone, hatua hiyo ya kuwataka raia wao kukutana kwa muzungumzo kwa muda wa siku tatu itahusu mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown na maeneo kadhaa ya kaskazini. Raia wanatakiwa kuzingatia hatua hiyo.

Kwa muda wa siku tatu, timu za wataalamu zitawahoji raia katika kutafuta wagonjwa wanaoweza kuwa wameambukizwa virusi vya Ebola na utaratibu unaotakiwa kufuata, hasa wakati wa sherehe za mazishi. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), maambukizi mapya yamefikia kiwango cha chini zaidi nchini Sierra Leone kwa muda wa miezi nane.

Mwanzoni mwa juma hili, rais wa Guinea Alpha Condé aliwatahadhari raia wake kuwa makini. “ Ugonjwa wa Ebola haujatokomezwa kabisa”, alisema rais Alpha Condé

Ugonjwa wa Ebola umeripotiwa nchini Liberia, siku chache baada ya viongozi kutangaza kuwa ugonjwa huo umetokomezwa. Lakini kugunduliwa kwa kesi mpya ya ugonjwa wa Ebola nchini Liberia, Jumamosi Machi 21, kesi ya kwanza tangu mwezi mmoja uliyopita, kumekua kama ilani kwa viongozi na raia. Kwa mujibu wa viongozi, mtu ambaye amebainika kuwa na virusi vya Ebola ni mwanamke ambaye inasadikiwa kuwa huenda aliambukizwa wakati alitembea kimapenzi na mwanamume ambae alinusurika baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola. Virusi vya Ebola vinabaki hai katika manii takriban miezi mitatu, baada ya mgonjwa kupona ugonjwa huo.