TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Habib Essid kwenye RFI: " tutatetea demokrasia yetu"

Baada ya shambulio lilioghrimu maisha ya watu katika makavazi ya kitaifa ya Bardo jijini Tunis, nchini Tunisia, Waziri mkuu wa Tunisia ameongea na RFI pamoja na gazeti la Le Figaro kuhusu udhaifu katika masuala ya kiusalama ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watalii ishirini wakiwemo raia watatu wa Ufaransa.

Waziri mkuu wa Tunisia, Habib Essid.
Waziri mkuu wa Tunisia, Habib Essid. AFP PHOTO / ARBI SOUSSI
Matangazo ya kibiashara

Habib Essid ameahadi kutetea demokrasia nchini Tunisia bila hita hivyo kutorejea kutumia njia ya kibabe.

RFI : Kwanini Islamic State, iliamua kuendesha shambulio Tunisia?

Habib Essid : Lengo kuu lilikuwa kukabiliana na kile ambacho tumekua tukifanya ili kuokoa msimu wa utalii na kudhoofisha sekta hii ambayo inakabiliwa na matatizo. Nchi yetu inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, na mkakati wa kigaidi umeongeza matatizo juu ya mengine. Kukosa msimu wa utalii, ni kuongeza idadi ya watu wasiokua na ajira. Na watu wasio na ajira pamoja na watu wenye hasira wanaweza kutumiwa kwa kutekeleza aina hii ya mashambulizi.

RFI : Nini unafahamu kuhusu magaidi hawa wawili ?

Habib Essid : Mmoja wa magaidi hao aliwahi kukamatwa na polisi. Alikua akifuatiliwa. Lakini aliweza kupotea, na alirudi kuonekana wakati alipokua kutekeleza uhalifu huo. Na mmoja kati ya magaidi hao alikua akiishi Libya.

RFI: Udhaifu gani wa usalama, ambao umetaja, ulikua wakati wa shambulio hilo?

Habib Essid : Inabidi tuwe wazi. Hata Paris, wakati wa shambulio dhidi ya gazeti la kila wiki la Charkie Hebdo, kulikueko na udhaifu. Mjini Tunis, mitambo ya ukaguzi iliyokua katika makavazi ya kitaifa ya Bardo haikufanya kazi vilivyo kwa wakati uliyotakiwa. Uchunguzi umeanzishwa. Waliohusika watabainika. Na hatua zitachukuliwa ili kuzuia hali hiyo isitokei tena.

RFI : Hatua gani hizo ?

Habib Essid : Mlolongo wa hatua. Tusubiri matokeo ya uchunguzi. Wale waote ambao hawakuwajibika kwa kazi yao wataadhibiwa*.

RFI : Naibu Spika alitangaza, baada ya shambulio hilo, kwamba askari polisi hawakuepo kwenye ngome zao wakati wa shambulio, inawezekana ?

Habib Essid : Sina taarifa sahihi kuhusu habari hiyo. Lakini inawezekana. Huenda walikua wakipumzika wakinywa kahawa. hawatakiwi kubaki sehemu moja, lakini wakati wa mapumziko ya kahawa askari polisi wengine wangelipaswa kuwarejelea kwenye ngome hiyo.