SENEGAL-SHERIA

Karim Wade ahukumiwa kifungo cha miaka sita jela

Kesi ya Karim Wade ilikuwa ikifuatiliwa na wengi kwa kipindi chote hiki
Kesi ya Karim Wade ilikuwa ikifuatiliwa na wengi kwa kipindi chote hiki AFP PHOTO / GEORGES GOBET

Mahakama nchini Senegal imemuhukumu Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo kifungo cha miaka sita jela na kutakiwa kulipa faini ya euro milioni 210 kwa kosa la kujitajirisha kinyume cha sheria na hii kufifiza ndoto zake za kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuondolewa kwa kosa la rushwa katika kesi iliokuwa ikimkabili Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal amepatikana na hatia ya kutjitajirisha kinyume cha sheria na hivyo kuhukumiwa kifungo cha mika sita jela na kutakiwa kulipa faini ya Euro miluoni 210

Wakati huo huo mahakama hiyo imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela washirika wa karibu wa Karim Wade hususan Bibo Bourgi, Alioune Samba Diassé, Mamadou Pouye huku wengine wakisafishwa na kuachiwa huru.

Wafuasi wa waziri huyo wa zamani katika serikali ya baba yake Abdoulaye Wade wamesikika wakipiga kelele mahakamani wakisema kwamba hii ni adhabu kubwa mno na kwamba hii ni kesi ya kisiasa ambapo jaji wa mahakama alilazimika kukatiza toleo la hukumu hiyo baada ya kuzomewe na umati wa watu waliokuwepo mahakamani kabla ya kuendelea baadae.

katika hali ya kupinga hukumu hii, baba wa Karim Wade ambae alikuwa ameelekea mahakamani kusikiliza hukumu hiyo amebaini maskitiko yake kutokana na maamuzi hayo ambayo ameyaita ya kisiasa.

Karim Wade alikuwa ameteuliwa na wafuasi wa chama cha PDS mwishoni mwa Juma lililopita kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2017, hivyo hukumu hii itamzuia kuwania nafasi hii.