SENEGAL-WADE-SHERIA-SIASA

Karim Wade ahukumiwa miaka sita jela

Karim Wade, apoteza matumaini ya kugombea katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017, baada ya Mahakama kumuhukumu kifungo cha mika sita jela.
Karim Wade, apoteza matumaini ya kugombea katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017, baada ya Mahakama kumuhukumu kifungo cha mika sita jela. AFP PHOTO / GEORGES GOBET

Mahakama ya Senegal imemuhukumu Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade, kifungo cha miaka sita jela na faini ya pesa za Senegal bilioni 138 (sawa na Euros milioni 210) kwa kosa la kujitajirisha kinyume cha sheria.

Matangazo ya kibiashara

Uamzi huu wa Mahakama unakata matumaini ya Karim Wade kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika mwaka 2017.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Dakar, Carine Frenk, kosa la rushwa ambalo ni miongoni mwa makosa aliyokua akikabiliwa Karim Wade limefutwa, lakini amepatikana na kosa la “ kujitajirisha kinyume cha sheria”. Karim Wade amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na faini ya Euros milioni 210.

Kwa upande wa watuhumiwa wenza kama Bibo Bourgi, Alioune Samba Diassé na Mamadou Pouye, wamepewa adhabu kubwa : kifungo cha miaka mitano jela na faini kubwa. Hata hivyo wawili miogoni mwao hawakjupatika na hatia, na wameachiliwa huru.

“ Adhabu hii ni kubwa”, wamelalamika wafuasi wa Karim Wade ambao walikua wamekuja kusikiliza uamzi wa Mahakama, huku wakibaini kwamba ni “ kesi ya kisiasa”.

Mkuu wa Mahakama amelazimika kukaa kimya kwa dakika chache kufuatia mayowe yaliyokua yakipigwa na wafuasi wa Karim Wade wakati alipokua akisoma uamzi wa Mahakama.

Kwa ishara za kupinga dhidi ya ukiukaji wa haki zake, Karim Wade hakuwa katika eneo wanakowekwa watuhumiwa. Hata hivyo, baba yake, Aboudalaye Wade, alikuja kusikiliza uamzi wa Mahakama. Rais huyo wa zamani alikataliwa kuhudhuria vikao wakati kesi ya mwanae ilipokua ikiendelea kwa kukataa "asivishawishisi vyombo vya sheria". Uwepo wake Jumatatu wiki hii Mahakamani imeonekana kama tukio kubwa. Abdoulaye Wade anatazamiwa kutoa tangazo katika masaa yajayo.

Kwa sasa wanasheria wa upande wa utetezi hawana nafasi ya kukata rufaa kwa sababu Mahakama inayoshughulikia kesi za utajiri haramu (Crei) haitoi nafasi ya kukata rufaa, lakini bado wanaweza kukata rufaa kwa Mahakama Kuu ya Senegal.

Karim Wade aliteuliwa, Jumamosi Machi 21 kuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha PDS katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwaka 2017. Kwa sasa uamzi huu unamzuia kugombea katika uchaguzi huo.