SENEGAL-WADE-SHERIA-SIASA

Mwanasheria wa Karim Wade aamua kukata rufaa

Karim Wade, mwana wa rais wa zamani wa Senegal ahukumiwa kifungo cha miaka sita jela, baada ya kukutwa na hatia ya kujitajirisha kinyume cha sheria.
Karim Wade, mwana wa rais wa zamani wa Senegal ahukumiwa kifungo cha miaka sita jela, baada ya kukutwa na hatia ya kujitajirisha kinyume cha sheria. AFP PHOTO / GEORGES GOBET

Nchini Senegal, mwanasheria wa Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal abdoulaye Wade ameamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu dhidi ya uamzi wa Mahakama.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Dakar, Carine Frenk, Karim Wade amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela na kutakiwa kulipa faini ya Euros milioni 210 baada ya kukutwa na hatia ya “ kashfa ya rushwa na kujitajirisha kinyume cha sheria”.

Mahakama nchini Senegal imemuhukumu Karim Wade, kifungo cha miaka sita jela na kutakiwa kulipa faini ya euro milioni 210 kwa kosa la kujitajirisha kinyume cha sheria na hii kufifiza ndoto zake za kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Wakati huo huo mahakama hiyo imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela washirika wa karibu wa Karim Wade hususan Bibo Bourgi, Alioune Samba Diassé, Mamadou Pouye huku wengine wakisafishwa na kuachiwa huru.

katika hali ya kupinga hukumu hii, baba wa Karim Wade ambae alikuwa ameelekea mahakamani kusikiliza hukumu hiyo amebaini maskitiko yake kutokana na maamuzi hayo ambayo ameyaita ya kisiasa.

baba wa Karim Wade amebaini maskitiko yake kutokana na maamuzi ya Mahakama dhidi ya mwanae Karim Wade, mamauzi ambayo ameyaita ya kisiasa.
baba wa Karim Wade amebaini maskitiko yake kutokana na maamuzi ya Mahakama dhidi ya mwanae Karim Wade, mamauzi ambayo ameyaita ya kisiasa. AFP Photo/Georges GOBET

Karim Wade alikuwa ameteuliwa na wafuasi wa chama cha PDS mwishoni mwa Juma lililopita kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2017, hivyo hukumu hii itamzuia kuwania nafasi hii.