TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Shambulio Tunis: wakuu wa polisi wafutwa kazi

Shambulio katika makavazi ya Bardo katika mji mkuu wa Tunisaia, Tunis, yamezimwa baada ya operesheni ya vikosi vya usalama,  tarehe 18 Machi mwaka 2015.
Shambulio katika makavazi ya Bardo katika mji mkuu wa Tunisaia, Tunis, yamezimwa baada ya operesheni ya vikosi vya usalama, tarehe 18 Machi mwaka 2015. .REUTERS/Zoubeir Souissi

Waziri mkuu wa Tunisia, Habib Essid, amechukua uamzi wa kuwafuta kazi wakuu wa polisi kadhaa, siku tano baada ya shambulio lililogharimu maisha ya watu 21 katika makavazi ya kitaifa ya Bardo jijiniTunis, nchini Tunisia. 

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilizua utata nchini humo, huku baadhi ya viongozi wakitwika lawama baadhi ya wakuu wa polisi kwamba hawakuwajibika wakati wa shambulio hilo aidha kabla ya shambulio hilo kutokea.

Serikali imechukua uamzi wa kuwafuta kazi wakuu kadhaa wa polisi. Uamzi huu unachukuliwa siku tano baada ya shambulio hilo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Habib Essid, ametaja mapungufu katika ulinzi wa makavazi ya kitaifa ya Bardo. Habib Essid, amesema aliona mapungufu hayo wakati alipotembelea eneo la tukio Jumapili jioni juma hili lililopita. Waziri huyo mkuu waTunisia amechukua hatua mara moja ya kuwafuta kazi wakuu wa polisi katika mji wa Tunis na kitongoji cha Bardo. Makamanda wengine pia wamefukuzwa kazi, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. Hati ya kukamatwa " ilitoa pia dhidi ya afisa wa polisi aliyekuwa akihusika na usalama wa Makavazi ya kitaifa ya bardo", imesema Ofisi ya Mashtaka.

Rais Béji Caïd Essebsi aliahidi kuanzisha uchunguzi kuhusu kutowajibika kwa baadhi ya vyombo vya usalama, baada ya kutambua kuwa kulikueko na udhaifu wa kiusalama.

" Kutokuwepo na askari polisi kwenye geti la Makavazi ya bardo, ambako kunapatikana jengo la Bunge la nchi hiyo, ni moja ya sababu za kushambuliwa kwa makavazi hayo", amesema rais Essebsi.

Waziri mkuu wa Tunisia ameahadi hatua katika Wizara ya Mambo ya ndani. Habib Essid anatambua kuwa viongozi " walipuuza" tishio ambalo limekua likiikabili Tunisia wakati wanajihadi wanaporejea nchini wakitokea Libya, Syria na Iraq.