SUDANI KUSINI-WATOTO

Unicef yapongeza hatuwa ya kuwaondowa watoto jeshini nchini Sudani Kusini

watoto jeshini wakati wa sherehe za kuwarejesha uraiani Februari 10, 2015, huko Pibor, jimbo la Joglei
watoto jeshini wakati wa sherehe za kuwarejesha uraiani Februari 10, 2015, huko Pibor, jimbo la Joglei AFP PHOTO/Charles LOMODONG

Shirika la Umoja wa Mataifa linalo hudumia watoto Unicef limesema takriban watoto 250 waliokuwa katika shughuli za kijeshi wamerejeshwa katika maisha ya kawaida huku wengine 400 wakitarajiwa pia kuachiwa katika hatuwa nyingine itayofuatia katika mradi wa kuwarejesha katika maisha ya kiraia watoto 300 uliotangazwa tangu januari iliopita.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika hilo la watoto duniani, Kuachiwa kwa watoto hao kunafikisha idadi ya watoto 1300 waliorejshwa katika maisnha ya kawaida tangu Januari 26 mwaka huu.

Watoto walioachwa walikuwa wamesajiliwa katika kundi la jeshi la kidemokrasia ya Sudani Kusini (SSDA) chama cha Cobra, kundi la waasi wa mashariki linaloongozwa na David Yau Yau ambalo Unicef ilifikia makubaliano ya mwezi Januari ya kuwaacha jumla ya watoto 3000, ikiwa ni moja kati ya operesheni muhimu za kuwarejesha katika maisha ya kawaida watoto na kuwaondowa jeshini.

Hata mamia ya watoto wanaendelea kuhudumu katika jeshi la serikali lakini pia katika kundi la waasi. Ijumaa juma lililopita Unicef iliituhumu serikali na waasi kuendelea kuwasajili watoto wadogo kwa nguvu na wengine kuwarteka katika kpindi chote hiki cha mapigano

Kulingana na shirika hilo la watoto duniani Unicef, takriban watoto 12.000 wengi wao wakiwa ni wavulana wamesajiliwa katika jeshi tangu mwaka 2014 nchini Sudani Kusini.

Sudani Kusini imekuwa ikikabiliana na makundi ya waasi tangu pale ilipojipatia uhuru wake mwexi Juni mwaka 2011, na baadae kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwezi Desemba mwaka 2013 kati ya wanajeshi tiifu kwa rais wa nchi hiyo Salva Kiir na makundi ua waasi wanaomtii makam wa rais wa zamani Riek Mashar.

Mapigano kati ya pande hizo mbili yanaoungwa mkono na makundi mbalimbali ya kikabila yanafuatiwa na machafuko ya raia yenye misingi ya kikabila.

Sudani Kusini ni taifa changa duniani iliogawika kutoka Sudani mwaka 2011 baada ya vita vya muda mrefu vya kutafuta uhuru (1983-2005) vita ambavyo watoto wengi walishirika katika kundi la SPLA lilitokea kuwa jeshi la taifa la Sudani Kusini.

Kutokana na shinikizo la kimataifa, Sudani Kusini ilijaribu kufanya juhudi za kuwarejesha katika maisha ya kawaida watoto wote waliokuwa jeshini na kuzuia ajira jeshini kwa watoto wadogo.

Lakini hali ilibadilika pale vita vilipoanza tena desemba 15 mwaka 2013 wakati rais Salva Kiir alipomtuhumu makam wake wa zamani Riek Machar kwamba amepnaga kufanya mapinduzi ya kijeshi.