MALI-AQMI-USALAMA

Boubacar Keita aahidi kuheshimu makubaliano wa amani

Ibrahim Boubacar Keita, rais wa Mali, wakati wa maadhimisho ya 54 ya uhuru wa Mali.Septemba 22 mwaka 2014.
Ibrahim Boubacar Keita, rais wa Mali, wakati wa maadhimisho ya 54 ya uhuru wa Mali.Septemba 22 mwaka 2014. Reuters/Joe Penney

Serikali ya Mali itafanya kila linalowezekana ili kutekeleza maazimio yaliyotolewa kwenye makubaliano ya amani na kundi la Tuareg, Rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita amebainisha msimamo huo jijini Algiers Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya mtu mmoja raia wa kawaida kuuawa na kukatwa kichwa siku chache zilizopita katika kanda ya Timbuktu kaskazini magharibi mwa nchi ya Mali, maafisa wa jeshi la Ufaransa wamethibitisha.

Tukio hilo limefanyika wakati mashirika ya kimisaada yaliyoko kaskazini mwa nchi hiyo, yamesema kundi la wapiganaji wa kiislamu wanaoungwa mkono na kundi la Al Qaeda Aqmi, wameendelea na hujuma zao Timbuktu na kuwaua mamia ya wananchi juma lililopita.

Jeshi la Ufaransa kwa upande wake limesema linafanya kila linalowezekana kuhakikisha amani na utulivu vinarejeshwa katika eneo hilo.