EBOLA-MSF-WHO-AFYA

Mvutano wajitokeza kuhusu mlipuko wa Ebola

Mtu aliyebainika hivi karibuni kuwa na virusi vya Ebola Liberia (amevalia nguo ya manjano), Monrovia, Machi 5 mwaka 2015.
Mtu aliyebainika hivi karibuni kuwa na virusi vya Ebola Liberia (amevalia nguo ya manjano), Monrovia, Machi 5 mwaka 2015. REUTERS/James Giahyue

Kumekuwa na Vita vya maneno kati ya shirika la madaktari wasio na mipaka MSF na shirika la afya ulimwenguni WHO kuhusiana na nani wa kulaumiwa kuhusiana na hatua za taratibu zilizochukuliwa kupambana na ugonjwa wa Ebola, ugonjwa uliozuka mwaka mmoja uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano unaotazamiwa kufanyika juma hili, wataalamu wa Shirika la madaktari wasio na mipaka wamesema wamejipanga kuhakikisha mbinu zilizochukuliwa pale ugonjwa huo wa Ebola ulipoenea kwenye mataifa ya Afrika magharibi, inaboreshwa.

Hata hivyo, kidole cha lawama kimeelekezwa dhidi ya jumuia ya kimataifa kwa kushindwa kutekeleza mikakati thabiti ili kuutokomeza ugonjwa huo hatari wa Ebola.

Baadhi ya mataifa ya Afrika ya Magharibi yaliathirika na ugonjwa huo. Maelfu ya raia walifariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Hata hivyo hivi karibuni, mtu mmoja amebainika kuwa na virusi vya Ebola nchini Lberia wakati, serikali ilikua ilitangaza siku chache kabla kuwa ugonjwa huo umetokomezwa nchi nzima.