Tembo wa Afrika huenda wakatoweka hadi miaka 20 ijayo
Imechapishwa:
Tembo walioko bara la Afika huenda wakatoweka kabisa katika kipindi cha miongo michache ijayo, wataalamu wameonya wakati huu mkutano wa kimataifa kuhusu wanyama pori na viumbe adimu duniani ukifanyika nchini Botswana.
Mkutano huu uliopewa jina Tembo wa Afrika, unafanyika katika mji wa kitalii wa Kasane ambapo wajumbe toka zaidi ya nchi 20 kutoka barani Ulaya, Afrika, Asia ikiwemo na China ambayo inatuhumiwa kuhusika na biashara haramu ya pembe za ndovu duniani.
Wataalamu wanasema, wanyama hawa huenda wakatoweka kabisa katika kipindi cha miaka mitano au kumi ijayo iwapo hali inayoshuhudiwa sasa itaendelea kuachiwa bila hatua kuchukuliwa.
Carlos Drews ambaye ni mkurugenzi wa shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanayama pori anayehusika na programu maalumu kuhusu viumbe hai, amesema wameridhishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi ya mataifa licha ya kuwa bado kuna hatari.