MISRI-MORSI-SHERIA

Wafuasi wa Morsi waendelea kukabiliwa na sheria

Wafuasi wa rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi, wakiandamana, Julai 3 mwaka 2014.
Wafuasi wa rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi, wakiandamana, Julai 3 mwaka 2014. REUTERS/Al Youm Al Saabi

Mahakama nchini Misri imewahukumu kifungo cha maisha jela wafuasi 23 wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Morsi.

Matangazo ya kibiashara

Hukumu hiyo iliyotolewa bila watuhumiwa kuwepo mahakamani, imetolewa na mahakama ya mji wa Giza huku tuhuma dhidi yao zikitajwa kuwa ni kushiriki katika maandamano yaliyokuwa yamepigwa marufuku katika kumuunga mkono rais huyo wa zamani wa Misri aliyeuzuliwa kwa nguvu na jeshi la nchi hiyo.

Itakumbukwa kuwa, miezi mitatu iliyopita, mahakama hiyo iliwahukumu adhabu ya kifo watu 188 kwa kuhusika na matukio ya mji wa Kerdasa nchini humo.

Faili la matukio ya mji wa Kerdasa, linahusiana na shambulizi lililofanywa dhidi ya kituo cha polisi katika mji huo nje kidogo ya jiji la Cairo na kupelekea askari polisi 13 kuuawa. Tukio hilo lilijiri ikiwa ni baada ya kuuzuliwa madarakani rais Morsi, suala lililoibua hali ya machafuko nchini humo.

Hata hivyo jumuiya ya kimataifa pamoja na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu vimmeendelea kulani hukumu ya kufungo dhidi ya masha jela dhidi ya wafuasi wa Mohamed Morsi.