CAR-USALAMA-SIASA

Rais Samba-Panza aendelea na jitihada za kuunganisha raia wake

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza ameahidi kufanya kila lilicho chini ya uwezo wake kuhakikisha uchaguzi ulio huru na wa haki unafanyika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza ameahidi kufanya kila lilicho chini ya uwezo wake kuhakikisha uchaguzi ulio huru na wa haki unafanyika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. REUTERS/Francois Lenoir

Rais Catherine Samba Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameahidi kufanya kila lilicho chini ya uwezo wake kuhakikisha uchaguzi ulio huru na wa haki unafanyika nchini mwake.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati mchakato wa mashauriano ya kitaifa nchini humo umefikia tamati yake baada ya wiki kadhaa ambapo tume iliyoundwa na rais wa nchi hiyo samba Panza imezunguuka nchi nzima kupata maoni ya wananchi.

Akizungumza na RFI, rais Samba Panza amesema kuwa zoezi hilo limekamilika kwa mafanikio makubwa hasa kwa kuwashirikisha wananchi katika kuamua mstakabali wa nchi yao.

Lengo la mashauriano hayo ni kuandaa Kongamano la kitaifa litakalofanyika mjini Bangui mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu kutathmini masuala kadhaa yanayohusiana na usitawi wa taifa hilo.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyotokea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kuangushwa kwa utawala wa François Bozize, viligharimu maisha ya maelfu ya raia na wengini wengi kuyahama makaazi yao.