TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Shughuzi za uzinduzi wa Makavazi ya Bardo zaahirishwa Tunis

Wakati wa maandamano ya kutoa rambrambi kwa wahanga wa shambulio dhidi ya makavazi ya kitaifa ya Bardo.
Wakati wa maandamano ya kutoa rambrambi kwa wahanga wa shambulio dhidi ya makavazi ya kitaifa ya Bardo. AFP PHOTO / FADEL SENNA

Shughuli za uzinduzi wa eneo la makumbusho, zilizokuwa zifanyike siku Jumanne wiki hii nchini Tunisia, zimeahirishwa hadi tarehe isiyojulikana bado. 

Matangazo ya kibiashara

Sherehe za kuwakumbuka wahanga 21 waliopoteza maisha mwishoni mwa juma lililopita katika shambulio lililotekelezwa na kundi la Islamic State zilifanyika mjini Tunis na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

Hata hivyo kumekuwa na mkanganyiko kuhusu sababu za kuahirishwa kwa tarehe ya uzinduzi wa eneo hilo.

Uongozi wa makavazi ya kitaifa ya Bardo umesema sababu za kiusalama ndio zimepelekea shughulihizo za ufunguzi kuahirishwa, wakati serikali yenyewe ikikanusha na kusema kwamba ni kutokana na ukarabati ambao bado haujakamilika.

Kundi la vijana wawili liliendesha shambulio majuma mawili yaliopita katika makavazi ya Bardo jiji Tunisia, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu 21 wengi wao waki watalii kutoka mataifa ya Ulaya.

Baada ya shambulio hilo kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu lilikiri kuhusika na shambulio hiolo. Hata hivyo rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi, aliapa kupambana na dhidi ya ugaidi nchini mwake.