DRC-MONUSCO-USALMA

Monusco yatazamiwa kuongezwa muda wa kubaki DRC

Rwindi, kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kakazini (DRC)wanajeshi wa Monusco kutoka India wakitumwa ili kuendesha operesheni dhidi ya makundi yenye silaha, Novemba 19 mwaka 2014.
Rwindi, kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kakazini (DRC)wanajeshi wa Monusco kutoka India wakitumwa ili kuendesha operesheni dhidi ya makundi yenye silaha, Novemba 19 mwaka 2014. Photo MONUSCO/Force

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Alhamisi wiki hii ili kupitisha azimio la kuongeza muda wa mwaka mmoja wa ziada kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa (Monusco) kubaki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya masuala ya majukumu ya kikosi hiki yameanza kuwa magumu kwa kuyaheshimu, wakati ambapo uhusiano kati ya ujumbe wa Umoja wa mataifa na serikali ya Congo umeingiwa na kasoro, kama kabla ya kila mzunguko wa uchaguzi.

Majukumu ya Monusco yaliibua mjada majuma ya hivi karibuni, wakati ambapo serikali ya Congo iliomba idadi ya wanajeshi wa Monusco ipunguzwe katika taifa hilo.

Kwa upande wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, usalama umeimarika. Lakini wafadhili wa nchi hiyo wanabaini kwamba mdororo wa kiusalama umeendelea kushuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo. Mauaji katika wilaya ya Beni mwezi Novemba mwaka 2014, vile vile mashambulizi ya mara kwa mara yanayoendeshwa na makundi mbalimbali ya watu wenye silaha kaskazini na kusini mwa mkoa wa Kivu au katika mkoa wa Katanga. Wote huo ni ushahidi tosha kwa Umoja wa Mataifa kwamba ni mapema nmo kuwaondoa wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Moja ya majukumu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (Monusco) yaliyowasilishwa miaka miwili iliyopita limeendelea kuzua utata. Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) kimepewa majukumu ya kuendesha operesheni peke yake dhidi ya makundi yenye silaha bila idhni ya serikali ya Congo. Hata hivyo serikali ya Kinshasa “ inapinga kwa niaba ya uhuru wake”, ameeleza mwanadiplomasia mmoja katika Umoja wa Mataifa mjini New York, akibaini kwamba wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanasisitiza kuwa operesheni dhidi ya makundi yenye silaha ziendeshwe kwa pamoja kati ya Monusco na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.