NIGERIA-CHAD-BOKO HARAM

Hatimaye uchaguzi mkuu kufanyika Nigeria,ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Jonathan na Buhari

Taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika,Nigeria linaingia katika uchaguzi leo jumamosi,uchaguzi wenye sura ya kipekee tangu taifa hilo kujipatia uhuru kufuatia ghasia za Boko haram,matatizo ya kiuchumi na suala sugu la rushwa.

Uchaguzi mkuu Nigeria unatazamiwa kushuhudia upinzani mkali kati ya raisi Goodlucjk Jonathan na Mohamadu Buhari
Uchaguzi mkuu Nigeria unatazamiwa kushuhudia upinzani mkali kati ya raisi Goodlucjk Jonathan na Mohamadu Buhari REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia miji ya kusini hadi kaskazini vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa moja za asubuhi tayari kwa wapigakura waliojisajili wapatao asilimia 68.8 wakitazamiwa kujitokeza kushiriki.

Tayari Goodluck Jonathan raisi wa naigeria anayewania kwa mara nyingine amewasili katika kijiji chake cha Utuoke katika jimbo la kusini Bayelsa akiwa na matuamaini ya kushinda awamu ya pili licha ya kasoro nyingi zinazomkabili.

Wakati huu mpinzani wake Muhammadu Buhari, yupo Daura, mji wa jimbo la kaskazini Katsina akitazamia kuingia madarakani kidemokrasia baada ya kuongoza kijeshi miaka ya 1980.