TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Kiongozi wa Aqmi Tunisia auawa

Polisi mbele ya makavazi ya kitaifa ya Bardo katika jiji la Tunis, Machi 19 mwaka 2015, siku moja baada ya shambulio. Tunis inahusisha shambulio hili kwa kundi la Aqmi.
Polisi mbele ya makavazi ya kitaifa ya Bardo katika jiji la Tunis, Machi 19 mwaka 2015, siku moja baada ya shambulio. Tunis inahusisha shambulio hili kwa kundi la Aqmi. REUTERS/Anis Mili

Halaiki ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis wakipinga ugaidi. Wakati huohuo, uchunguzi kuhusu shambulio la makavazi ya kitaifa ya Bardo umeendelea.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya viongozi wa kigeni, akiwemo rais wa Ufaransa, François Hollande, wameshiriki maandamano haya.

“ Tutaandamana kwa kuiunga mkono Tunisia na maadili inayowakilisha kwa nchi za Kiarabu", amesema rais wa Ufaransa.

Mamia kwa maelfu ya watu, watu 40,000 kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, waliwasili mapema asubuhi kando na makavazi ya kitaifa ya Bardo jijini Tunis. Umati wa watu wenye kuvutia, ambao walikua wakishikilia bendera na ambao waliandamana kilomita nyingi wakianzia kwenye mmoja wa milango ya Madina.

Wimbi linaloundwa na watoto, wazee na vijana wa tabaka zote. Wananchi wa kawaida lakini pia wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi wa asasi mbalimbali na vyama vya siasa, wote wameungana dhidi ya ugaidi. Waandamanaji hawa wamekua na mabango yanayoandikwa " Sisi ni Bardo", " Hapana kwa ugaidi" na walikubaliana kutuma ujumbe ufuatayo : " Hatutakubali kushawishiwa". Maneno yalirudiliwa mara kwa mara. Wametuma pia ujumbe kwa wageni: " Msiwe na hofu ya kuja Tunisia", wakitolea wito watalii kuja nchini mwao.

Kulionekana idadi kubwa ya vikosi vya usalama wakati wa maandamano haya, huku helikopta zikitoa ulizi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Tunis. Usalama uliimarishwa kufuatia kuwepo kwa viongozi kadhaa wa kigeni katika maandamano haya, hususan rais wa Ufaransa François Hollande, lakini pia marais wa poland, Bronislaw Komorowski na Palestina, Mahmoud Abbas.

Hayo yakijiri afisa mmoja wa wizara ya mambo ya ndani, amebaini Jumapili Machi 29 kwamba wanamgambo tisa wa kiislamu wameuawa na vikosi vya Tunisia katika mkoa wa Gafsa, kusini mwa nchi. Loqman Abou Sakhr, kiongozi wa kundi la Aqmi, ni miongoni mwa waliouawa.

Watu hao tisa wamekua wakichukuliwa kama magaidi hatari nchini Tunisia. Loqman Abou Sakhr, ni miongoni mwao, ambaye alikua akitafutwa kwa udi na uvumba nchini Tunisia. Waziri mkuu wa Tunisia Habib Essid amethibitisha kifo chake.

Mpiganaji huyo, mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini, alikua kiongozi wa kundi la Aqmi lenye uhusiano na kundi la Al Qaeda. Alikua akijulikana kwa jina la Oba ibn Nafa, ambalo ni jina la muanzilishi wa Msikiti wa Kairouan, ambaye alikua kiongozi wa kijeshi na mtu ambaye alisambaza Uislamu katika karne ya saba.

Loqman Abou Sakhr ameuawa akiwa na wanamgambo wengine wanane wa kiislamu katika eneo lenye milima la mkoa wa Gafsa, kusini mwa Tunisia, kwenye umbali wa zaidi ya kilomita hamsini na mpaka wa Algeria.

Takribani miaka miwili, kundi la Aqmi nchini Tunisia limeua mamia ya watu na wanajeshi kadhaa wa Tunisia kwa kutumia mabomu yanayotengenzwa kienyeji.

Wanajeshi hao waliuawa katika matukio mbalimbali, hususan mashambulizi ya kuvizia yalioendeshwa na kundi hilo na wengine walichinjwa katika mlima wa Chambi, kwenye mpaka na Algeria, mwezi Julai mwaka 2013. kundi la Okba ibn Nafa lina zaidi ya wapiganaj isitini.

Serikali ya Tunisia inalihusisha kundi la Aqmi kwa shambulio lililotekelezwa katika makavazi ya kitaifa ya Bardo jijini Tunis, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu ishirini na mmoja, wakiwemo raia wanne wa Ufaransa.

Hata hiivyo kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu lilikiri kutekeleza shambulio hilo. Lakini serikali ya Tunisia imeendelea kuhakikisha kwamba shambulio hilo lilipangwa na Loqman Abou Sakhr.