TUNISIA-UGAIDI-MAANDAMANO-USALAMA

Mamia kwa maelfu ya watu waandamana dhidi ya ugaidi Tunis

Moja ya mabango yakionyesha mshikamano kwa waathirika wa mashambulizi katika makavazi ya kitaifa ya Bardo, Machi 18 dernier.
Moja ya mabango yakionyesha mshikamano kwa waathirika wa mashambulizi katika makavazi ya kitaifa ya Bardo, Machi 18 dernier. www.facebook.com

Tangu Jumapili mchana Machi 29, mamia kwa maelfu ya raia wameandamana katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis. Maandamano haya ni ya amani kwa kusema hapana kwa ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya viongozi wa kigeni, akiwemo rais wa Ufaransa, François Hollande, wameshiriki maandamano haya.

“ Tutaandamana kwa kuiunga mkono Tunisia na maadili inayowakilisha kwa nchi za Kiarabu", amesema rais wa Ufaransa.

Mamia kwa maelfu ya watu, watu 40,000 kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, waliwasili mapema asubuhi kando na makavazi ya kitaifa ya Bardo jijini Tunis. Umati wa watu wenye kuvutia, ambao walikua wakishikilia bendera na ambao waliandamana kilomita nyingi wakianzia kwenye mmoja wa milango ya Madina.

Wimbi linaloundwa na watoto, wazee na vijana wa tabaka zote. Wananchi wa kawaida lakini pia wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi wa asasi mbalimbali na vyama vya siasa, wote wameungana dhidi ya ugaidi. Waandamanaji hawa wamekua na mabango yanayoandikwa " Sisi ni Bardo", " Hapana kwa ugaidi" na walikubaliana kutuma ujumbe ufuatayo: " Hatutakubali kushawishiwa". Maneno yalirudiliwa mara kwa mara. Wametuma pia ujumbe kwa wageni: " Msiwe na hofu ya kuja Tunisia", wakitolea wito watalii kuja nchini mwao.

Kulionekana idadi kubwa ya vikosi vya usalama wakati wa maandamano haya, huku helikopta zikitoa ulizi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Tunis. Usalama uliimarishwa kufuatia kuwepo kwa viongozi kadhaa wa kigeni katika maandamano haya, hususan rais wa Ufaransa François Hollande, lakini pia marais wa poland, Bronislaw Komorowski na Palestina, Mahmoud Abbas.

Algeria ambayo imeendela kupambana dhidi ya ugaidi kwenye mpaka wake na Tunisia, imeonesha mskikamano wake kwa taifa la Tunisia dhidi ya ugaidi.
Wameshiriki pia katika maandamano hayo mawaziri wa nchi kadhaa za Ulaya, waziri mkuu wa Italia, waziri wa mambo ya nje wa Uhispania, waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani pamoja na waziri mkuu wa Algeria. Viongozi hawa wote watazindua mnara wa kumbukumbu kwa heshima ya waathirika wa shambulio lililoendeshwa katika makavazi ya Bardo na kuua watu 21, wengi wao wakiwa watalii.