NIGERIA-INEC-UCHAGUZI-UHESABUJI-SIASA

Zoezi la kuhesabu kura limeanza Nigeria

Afisaa wa Tume Huru ya Uchaguzi akikagua visanduku kilio na kura ziliyopigwa Jumamosi, Machi 28, katika jimbo la Katsina, wakati ambapo kura zimeendelea kupigwa Jumapili Machi 29 mwaka 2015 katika maeneo 300.
Afisaa wa Tume Huru ya Uchaguzi akikagua visanduku kilio na kura ziliyopigwa Jumamosi, Machi 28, katika jimbo la Katsina, wakati ambapo kura zimeendelea kupigwa Jumapili Machi 29 mwaka 2015 katika maeneo 300. AFP/PIUS UTOMI EKPEI

Matokeo ya awali yamepangwa kutangazwa saa 48 baada ya uchaguzi, na zoezi hilo litaahirishwa kufuatia namna uchaguzi ulivyofanyika kwa siku mbili mfululizo kutokana na kasoro za kiufundi, lakini uhesabuji wa kura unaendelea vizuri.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuhesabu kura linashuhudiwa pia katika kitongoji cha Yaba nje kidogo ya mji wa Lagos ambapo visanduku viliyojaa kura ziliyopigwa vilikua vikisafirishwa hadi kwenye shule moja ambayo itatumiwa kama kituo cha ukusanyaji kwa ajili ya vituo vyote vya kupigia kura katika mji kijiji cha Mainland Lagos. Maafisa wa Tume ya Uchaguzi, vikosi vya usalama laikini pia waangalizi wa mashirika mbalimbali wapo katika kituo hicho.

Tume ya uchaguzi iliahirisha uchaguzi katika maeneo kadhaa ya Nigeria kwa sababu ya hitilafu ya mitambo ya kutambua vitambulisho vya kupigia kura.

Awali msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Kayode Idowe. amesema kuna maeneo mashine za kusoma kadi za kupigia kura hazikutumiwa kabisa kwa sababu ya hitilafu ya teknolojia.

 Rais Goodluck Jonathan pia aliathiriwa na tatizo hili na kulazimika kutimia njia ya kawaida kabla ya kupiga kura hapo mwishoni mwa juma hili.

Hata hivyo, katika maeneo ambayo zoezi hili lilikwenda vizuri kura zimeanza kuhesabiwa leo Jumapili.

Chama tawala PDP kimeishtumu Tume ya Uchaguzi kwa kutofanya maandalizi ya mapema kuhusu mitambo hii, huku muungano wa upinzani APC ukisisitiza umuhimu wa utumizi wa mitambo hiyo ili kuepuka wizi wa kura.

Ushindani mkubwa ni kati ya rais Goodluck Jonathan na kigogo wa upinzani Muhamdu Buhari.

Wachambuzi wa siasa nchini Nigeria wanasema huu ndio uchaguzi wenye ushindani mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika taifa hilo tangu ilipojipatia uhuru wake mwaka 1960.

Uchaguzi huu uliahirishwa kwa muda wa wiki sita ili kutoa muda kwa jeshi la serikali na yale ya nchi jirani ya  Chad, Niger na Cameroon kupambana na kundi la Boko Haram Kaskazini mwa nchi hiyo.

Rais Jonathan na mpinzani wake Buhari wameahidi kuhakikisha kuwa ghasia hazitokei nchini humo wakati wa zoezi hili na baada ya upigaji kura na watakubali matokeo.