NIGERIA-NIGER-CHAD-BOKO HARAM-USALAMA

Boko Haram yapoteza kijiji cha Abadam

Majeshi ya Niger na Chad yameendesha mashambulizi dhidi ya Boko Haram katika kijiji cha Abadam, kwenye umbali wa zaidi ya kilomita hamsini na mji wa Damasak.

Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika ardhi ya Nigeria dhidi ya Boko Haram, Februari 3 mwaka 2015.
Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika ardhi ya Nigeria dhidi ya Boko Haram, Februari 3 mwaka 2015. AFP PHOTO / STEPHANE YAS
Matangazo ya kibiashara

Majeshi hayo yamebaini kwamba yamedhibiti kijiji hicho na yanaendelea na mapambano hadi katika mji wa Malam-fatouri.

Hata hivyo majeshi hayo ya Niger na Chad yamebaini kwamba yamefanikiwa kuwaua zaidi ya wapiganaji hamsini wa Boko Haram, na kukiri kuwapoteza wanajeshi wawili na wengine 16 kujeruhiwa.

Majeshi ya Chad, Niger, Nigeria na Cameroon yameendelea na vita dhidi ya Boko Haram, na yameapa kutokomeza kundi hilo, ambalo limekua likihatarisha usalama katika nchi ya Nigeria na baadhi ya maeneo ya nchi jirani.

Boko Haram imekua ikiendesha mashambulizi ya hapa na pale katika maeneo mengi ya nchi ya Nigeria. Hata hivyo kundi hili limeendelea kupoteza maeneo hayo, baada ya majeshi ya nchi hizo nne kuanzisha mashambulizi.

Raia wengi waliangamia katika mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria na nchi jirani.