AFRIKA-ALGERIA-DIPLOMASIA-USALAMA

Jacob zuma ziarani Algiers

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Reuters/Nic Bothma/Pool

Rais wa Afrika kusini aliwasili katika mji mkuu wa Algeria, Algiers Jumatatu jioni kwa ziara ya siku tatu. Jacob Zuma anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo na rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ambayo itagubikwa hasa na masuala ya usalama, inatokea baada ya marais wa Mali, Niger na Zimbabwe kufanya zira nchini Algeria.

Ni ziara ya pili ya rais wa Afrika Kusini ndani ya kipindi cha miaka miwili. Jacob Zuma pamoja na Abdelaziz Bouteflika watazungumzia masuala ya amani na usalama barani Afrika, kama jinsi alivyofanya rais wa Algeria na wenziye wa Mali, Niger pamoja na Robert Mugabe. Mazungumzo hayo yatagubikwa hasa na ugaidi, mgogoro nchini Libya lakini pia suala la silaha.

Algeria na Afrika Kusini ni nchi mbili za kwanza katika masuala ya kijeshi barani Afrika. Makubaliano ya ulinzi yalisainiwa kati ya nchi hizi mbili mwaka 1999, makubaliano ambayo yanaruhusu nchi hizo mbili kuuziana silaha kwa urahisi zaidi.

Lakini Algiers na Pretoria, ambao wana ushirikiano wa kihistoria, wanataka, kwa mujibu wa taarifa rasmi, kutafuta aina mpya ya ushirikiano. Jacob Zuma ameambatana katika ziara hii na mawaziri wake wanne au watano.

Hatimaye, Algeria na Afrika Kusini, wanataka kujaribu kurekebisha kile wanachokiita kubaguliwa kwa bara la Afrika katika nyanja ya kimataifa. Mkakati ambao unahusisha raia wa Algeria kufuatia kuimarika kwa uhusiano wa kidiplomasia na majirani zao wa Kiafrika.