NIGERIA-INEC-UCHAGUZI-SIASA

Kambi ya Muhammudu Buhari yasheherekea ushindi

kambi ya Muhammadu Buhari yasheherekea ushindi wakati matokeo ya uchaguzi wa urais yamekua yakiwasili kwa mwendo wa kinyonga, Machi 31 mwaka
kambi ya Muhammadu Buhari yasheherekea ushindi wakati matokeo ya uchaguzi wa urais yamekua yakiwasili kwa mwendo wa kinyonga, Machi 31 mwaka REUTERS/Joe Penney

Mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari anaonekana kuongoza kati ya majimbo 31 kwa jumla ya majimbo 36 dhidi ya mshindani wake rais anaye maliza muda wake Gooluck Jonathan.

Matangazo ya kibiashara

Kambi ya Buhari inaongoza kwa asilimia kubwa dhidi ya kambi ya mshindani wake Goodluck Jonathan, na tayari wameanza kusheherekea ushindi.

Kulingana na kura zilizohesabiwa kutoka majimbo 31 kwa jumla ya majimbo 36, Muhammadu Buhari ameshinda, na tayari matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya yametangazwa. Mpaka sasa chama cha APC cha Muhammadu Buhari kimepata kura milioni 10.8 katika baadhi ya majimbo ya kaskazini mwa Nigeria, hususan katika majimbo ya Adamawa, Kano na Kaduna, huku chama cha rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan kikipata kura milioni 11.8 Kusini mwa nchi hiyo katika majimbo ya Enugu, Bayelsa na Rivers.

Kwa jumla ya kura zilizohesabiwa Muhammadu Buhari anaongoza kwa kura milioni 2.7 dhidi ya mshindani wake rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan.

Duru kutoka Nigeria zimebaini kwamba rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan amempongeza kwa simu Muhammadu Buhari.

Buhari akiri kushinda uchaguzi wa urais Nigeria.
Buhari akiri kushinda uchaguzi wa urais Nigeria. Reuters

Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Kaskazini mwa Nigeria.

Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, kati ya mwaka 1983-1985.

Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi nchini Nigeria, India, Marekani na Uingereza .

Buhari aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa mfuko wa Amana ya Mafuta. Inasemekana kuwa Buhari ni mtu kaidi, hakubali kushindwa.

Naye rais anayemaliza muda wake Goodluck Jonathan, ni mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini mwa Nigeria.