Mali : Mujao yakiri shambulio dhidi ya lori la CICR

Mji wa Gao ukitazamwa kutoka juu.
Mji wa Gao ukitazamwa kutoka juu. RFI/David Baché

Visa vya mashambulizi ya kigaidi vimekua sugu nchini Mali. Juma lililopita, nyumba moja ilishambuliwa katikati mwa mji wa Gao.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo lori la shirika la msalaba mwekundu (CICR) limeshambuliwa, na kusababisha mtu mmoja kuuawa na mwengine kujeruhiwa.

Lori hilo la CICR lilikua likitokea katika mji wa Gao na lilikua likelekea nchini Niger kutafuta vifaa vya vya matibabu vya hospitali ya mji huo. Kwa mujibu wa shirika hilo, lori hilo lilishambuliwa na watu wengi wenye silaha, kwenye umbali wa zaidi ya kilomita arobaini na mji wa Gao kwenye barabara ya Ansongo. Dereva wa lori hilo ameuawa katika shambulio la kuvizia. Mtu mwengine amejeruhiwa katika shambulio hilo, na wakati huu amelazwa katika hospitali ya Gao. Gari ilichomwa moto.

Kundi la Mujao limekiri kuhusika katika shambulio hilo. Kundi hilo limedhibiti eneo la kaskazini mwa Mali tangu mwaka 2012. Mujao ni tawi la kundi la kigaidi la al-Mourabitoune. Kundi hili limekua likiendesha harakati zake kaskazini mwa Mali, na hivi karibuni lilikiri kuhusika katika shambulio lililogharimu maisha ya watu watano katika mji wa Bamako, mwanzoni mwa mwezi wa Machi.