MAREKANI-KENYA-DIPLOMASIA

Obama kwenye ardhi ya Kenya mwezi Julai

Barack Obama anatazamiwa kuizuru Kenya mwezi Julai.
Barack Obama anatazamiwa kuizuru Kenya mwezi Julai. Reuters/路透社

Rais wa marekani Barack Obama anatazamiwa kufanya ziara rasmi nchini Kenya mwezi Julai mwaka huu. Ziara hii kwenye ardhi ya nchi alikozaliwa babake ilikua ikisubiriwa na raia wa Kenya tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani miaka sita iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani atahudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu ujasirimali, utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.

Tangu awe Rais wa Marekani, Barack Obama hajawahi kuzuru taifa hilo la Afrika Mashariki kama Rais.

Maelfu ya viongozi wa makampuni watashiriki mkutano huo.barack Obama alizuru Kenya akiwa seneta mnamo mwaka 2006.

Babake Obama alisomea Marekani na hatimaye kurejea Kenya baada ya Obama kuzaliwa.

Obama alizuru mataifa kadhaa ya Afrika ikiwemo Tanzania mnamo mwaka 2013 bila kuzuru Kenya. Hangeliweza kuizuru Kenya, nchi ambayo mwaka 2006, aliitaja kua imekithiri kwa rushwa.

Hata hivyo rais Obama alichelewa kuizuru Kenya kutokana na kesi ya tuhuma ya uhalifu dhidi ya binadamu iliyokua ikimkabili rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Ziara hii ya kihistoria itafanyaka mwishoni mwa mwezi Julai, lakini mpaka sasa Ikulu ya White House imejizuia kutoa taarifa zaidi kuhusu ziara hii ya Barack Obama. Haijaaminika iwapo Barack Obama atamtembelea yule anayemchukulia kama bibi yake, mke wa tatu wa babu yake, ambaye anaishi katika kijiji kimoja magharibi mwa Kenya.