KENYA-SHAMBULIo-GARISSA-USALAMA

Kenya : shambulio katika Chuo Kikuu cha Garissa

Wanajeshi wa kenya kwenye eneola shambulio, Garissa, Aprili 2 mwaka 2015.
Wanajeshi wa kenya kwenye eneola shambulio, Garissa, Aprili 2 mwaka 2015. REUTERS

Watu wenye silaha wameendesha shambulio Alhamisi asubuhi wiki hii katika Chuo kikuu cha Garissa, mashariki mwa Kenya, kilomita 150 kutoka kwenye mpaka wa Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Askari polisi wametumwa katika eneo la shambulio, ambapo milipuko inaendelea kusikika. Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, watu wawili wameuawa na wengine wanne wamejurihiwa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, shambulio hilo lilianza saa za swala mapema asubuhi, kwenye majira ya saa kumi na moja na nusu leo Alhamisi. Idadi ya watu walioendesha shambulio hilo haijajulikana

Kwa mujibu wa gazeti la Kenya la The Standard, wanafunzi waliofaulu kuondoka chuoni hapo, wamesema waliwaona watu watano wenye silaha.

Kwa mujibu wa polisi ya Kenya, watu hao wenye silaha, walianza kufyatua risase walipoingia chuoni hapo. Walinzi wawili wameuawa. “ Mpaka sasa milio ya risasi imeendela kusikika katika Chuo kikuu cha Garissa, lakini ni vigumu kujua nani anayemrushia risasi mwengine”, mwakilisi wa polisi eneo hilo amesema, huku akibaini kwamba washambuliaji wamewateka nyara wanafunzi.

Wakati walinzi wa Chuo kikuu cha Garissa waliposikia milio ya kwanza ya risasi waliweza kujibu, lakini walizidiwa nguvu, na washambuliaji hao waliweza kufaulu kuingia katika chuo kikuu hicho.

Hata hivyo polisi na jeshi vimefaulu kuingia katika chuo kikuu Garissa, lakini mpaka sasa milio ya risasi na milipuko vimendelea kusikika.