NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Mahammadu Buhari aapa kutokomeza Boko Haram

Muhammadu Buhari amechaguliwa kuwa rais Nigeria, Machi 2015.
Muhammadu Buhari amechaguliwa kuwa rais Nigeria, Machi 2015. AFP PHOTO /STRINGER

Katika hotuba yake, Rais mteule wa Nigeria, Mahammadu Buhari, ameahidi kuhakisha kundi la Boko Haram linaangamizwa katika utawala wake. Mahammadu Buhari ameahidi pia kupambana na rushwa ambayo imekithiri nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Katika kampeni zake Mahammadu Buhari aliahidi kupambana na changamoto zinazo ikalibili taifa la Nigeria, hususan rushwa na suala la mdororo wa usalama ambalo limekua gumzo nchini Nigeria.

Rais mteule wa Nigeria ameapa kulitokomeza kundi hilo la Boko Haram kwa njia zote, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na mataifa jirani.
Baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi na Tume huru ya Uchaguzi (Inec) Jumatano wiki hii, Mahammadu Buhari alisema ushindi wake umedhihirisha kuwa nchi yake imekua kidemokrasia.

Kwa mara ya kwanza katika mabadiliko yake ya kidemokrasia yanayoendelea, Nigeria sasa imeanza kushuhudia wakati wa kihistoria tangu kuwepo kwake. Tangu kupata uhuru mwaka 1960, koloni hii ya zamani ya Uingereza ilishuhudia vita vya wenyewe toka mwaka 1967 hadi 1970. Vita hivyo vilisababisha vifo vya zadi ya watu milioni, huku kukishuhudiwa mapinduzi sita, na miaka 28 ya utawala wa kijeshi.

Kuanzishwa mwaka 1990 kwa Katiba mpya kulipelekea kuwepo na misingi ya kidemokrasia kwa taasisi ya Bunge na uchaguzi wa rais wa kwanza, raia wa kawaida, aliyejulikana kwa jina la Olusegun Obasanjo, mwanzilishi wa chama kikuu cha kwanza cha PDP. Baada ya miaka kumi na tano chama cha PDP kikiwa madarakani, raia wa Nigeria leo wanahudhuria hatua ya mageuzi katika maisha yao ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa urais wa mgombea kutoka muungano wa vyama vya upinzani.