Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Shambulizi la kigaidi dhidi ya Chuo kikuu cha Garisa, na Uchaguzi mkuu wa Nigeria, pia mkataba juu ya Nyuklia wa Iran

Sauti 21:43

Wananchi wa Kenya juma hili waliomboleza vifo vya watu 147 waliouawa katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na Al Shabab katika chuo kikuu mjini Garisaa kaskazini mashariki mwa Kenya; rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyata akaahidi kuwekeza nguvu zaidi kupambana na ugaidi katika nchi hiyo.Rais mteule nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameahidi kuliondolea taifa lake na tatizo la ugaidi wa kundi la Kiislam la Boko Haram, na toa wito wa maridhiano na wapinzani wa kisiasa na kuahidi kurejea kwa utawala utakaowawakilisha wananchi wote wa Nigeria.Mazungumzo baina ya nchi za magharibi na Iran kuhusu ufuaji wa nishati ya nyuklia hatimaye yamefikia makubaliano ya awali mjini Lausanne nchini Uswisi hapo jana.